0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 9, 2018 ameonya watu wanaopanga kuandamana akidai kuwa huu sio muda wa maandamano bali ni muda wa kujenga taifa.
Rais Magufuli amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanapenda kuona Tanzania ikiwa na migogoro kila siku na wanafurahi kuona watu wanaandamana mabarabarani.
Wapo watu wangependa nchi hii kila siku tuwe na migogoro, Wapo watu ambao wameshindwa kufanya siasa za kweli, wangependa kila siku tupo mabarabarani tunaandamana.
 Watu wao wanahamia huku wao wanataka wabaki wanaandamana kule, nimeshasema ngoja waandamane wataniona, kama kuna baba zao wamewatuma watakwenda kuwasimulia vizuri,“amesema Rais Magufuli leo Machi 9, 2018 kwenye uzinduzi wa tawi la benki ya CRDB mjini Chato.
Kauli hiyo ya Rais Magufuli imekuja wakati kukiwa na taarifa zikizagaa mitandaoni kuwa kuna watu wanapanga maandamano yasiyo rasmi.
Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewataka Watanzania kufanya kazi na kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki cha mwanzo hadi tutakapofika kwenye nchi ya asali.
Wakati huo huo  Rais John Magufuli amesema licha ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei anakaribia kustaafu ameahidi kumpatia nafasi katika Serikali ya Awamu ya Tano.
 “Kimei wewe ustaafu tu lakini nasema nafasi bado zipo. Muda wako unamalizika CRDB lakini Serikalini bado unaweza kufanya kazi ndani ya Serikali bado upo na ninakuahidi asilimia 100,” amesema Rais Magufuli.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top