0
Kikosi cha Usalama Sports Club.
MKUU wa upelelezi wa makosa ya jinai wa mkoa wa Manyara (RCO) Joshua Mwafulango ameeleza kuendelea na mikakati ya kuhakisha timu ya usalama sc inatwaa ubingwa wa ligi ya mkoa Manyara na isonge mbele Katika ligi ya Mabingwa mikoa (RCL).
Akizungumza baada ya pambano mkali wa kundi B ya ligi hiyo kati ya timu ya Usalama Sc ambayo ilichapa bila huruma mabao 5-2 timu ya Halmashauri fc mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa chuo cha ufundi Nangwa wilayani Hanang alisema timu hiyo inaonyesha kufanya vizuri kutokana na wachezaji kujituma baada ya kushirikiana na uongozi kwa karibu.
"Atutarajii kwamba timu itaenda mbele alafu itasimama kwa sababu mipango iliyopangwa ni madhubuti kiasi kwamba timu ilivyoanza mwanzoni hadi mwisho itakuwa ni moto" alisema Mwafulango.
Kwa upande wake kocha wa Usalama Sc Ryoba Kanyenye aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kuibuka na ushindi mnono katika mchezo wa kwanza huku akiahidi kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwa upande wa timu yake.
"Ushindi wa 5-2 ni suala la wachezaji kujitolea,kujituma na wameamua kufanya kazi,tumejiandaa kwa muda mrefu na kutumia rasilimali nyingi sana hivyo kila mchezo kwetu ni fainali" alissma Kanyenye.
Katika mchezo huo magoli ya Usalama sc yalifungwa na wachezaji David Shebe dk 9,Makame Othman dk 55,Majaliwa Juma dk 62,Hamadi Hamisi dk 71 na Salum Juma dk 90 huku kwa upande wa Halmashauri fc magoli yakifungwa na Martin Maira dk 70 na Mlangida Martin dk 89.
Ligi ya mkoa wa Manyara inashirikisha jumla ya timu 9 Katika makundi mawili ya A na B  zinazochuana vikali kutafuta  timu tatu ambazo  zitafuzu kuingia hatua ya sita bora kutoka katika kila kundi.
Kundi A kuna timu za Gwadaat fc,Bm fc,Magugu rangers fc,Fire stone na Morning star fc.
Wakati kundi B kuna timu za Red star fc,Nangwa fc,Halmashauri fc na Usalama Sc.Ligi hiyo inachezwa Katika uwanja wa chuo cha ufundi Nangwa Katesh wilayani Hanang.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top