0
Image result for riadha  MANYARA 
Chama cha riadha mkoa wa Manyara kimeanza mchakato wa kutafuta wanariadha watakaoiwakilisha mkoa huo katika Mashindano ya riadha taifa yanayotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi juni.
Akiongea na WALTER HABARI mwenyekiti wa chama cha riadha mkoa wa Manyara mwalimu Safari Ingi alisema wanatarajia kuandaa mashindano ya mbio za wazi katika ngazi ya mtaa mpaka wilaya kwa ajili ya kutafuta washindi ambao wataenda kushindana katika ngazi ya mkoa aprili 24 kupata timu kamili.
Alisema mbio ambazo zitashindaniwa ni za uwanjani mita 100,mita 200,400,800,1500,5000 na 10,000 huku akiweka wazi kuwa itawashirikisha watu wazima pamoja na wanafunzi.
 Alisema  lengo lao ni kuhakiksha wanaibua vipaji vya wanariadha ambao bado vipaji vyao havijaonekana na kuweka wazi kuwa timu itakayochaguliwa itaenda kuiwakilisha mkoa katika mashindano ya taifa ya riadha itakayofanyika mwishoni mwa mwezi juni au julai mwanzoni pia kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki ya 2020 nchini Japan.
"Sisi tumejipanga kama Manyara kwamba lazima tutoe wanariadha wasiopungua kumi ambao ni bora na wilaya zote nimeshawaambia mchakato huu ufanyike kwa halali na tupate watu wazuri watakao iletea heshima mkoa wetu" alisema mwalimu Ingi.
Alisema zawadi mbali mbali zitatolewa kwa washindi kuanzia ngazi ya mitaa,kijiji,kata,tarafa hadi wilaya huku akiwaomba wanariadha wanaochipukia kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top