0
Nakusogezea Tahadhari kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA) imesema kuanzia usiku wa leo March 1, 2018  hadi March 2, 2018
kutakuwa na vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi ya nyanda za Juu
Kaskazini Mashariki.



Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo katika Channel ya TMA imetaja maeneo hayo kuwa ni mkoa wa Arusha, Manyara na Kilimanjaro ambapo mvua hizo itazidi Milimita 50 ndani ya saa 24 huku ilieleza hali hiyo inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua.


TMA imewashauri wakazi wa maeneo husika kuchukua tahadhari na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zinazotolewa.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top