0


Image result for SIMBA VS AL MASRYMCHEZO wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba SC na Al Masry ya Misri umemalizika kwa sare ya 2-2 usiku huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Matokeo hayo yanamaanisha Simba SC wanahitaji kwenda kupigania ushindi wa ugenini siku 10 zijazo mjini Cairo, Misri ili kusonga mbele. 
Mchezo huo ulisimama kwa takriban nusu saa kuanzia dakika ya 83 kufuatia umeme kukatika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam timu hizo zikiwa zimefungana mabao 2-2.
Refa Hando Helpus aliyesaidiwa na Zakjele Thusi na Athenkosi Ndongeni wote kutoka Afrika Kusini alilazimika kusimamisha mchezo huo baada ya umeme kukatika ghafla dakika ya 83, dakika 10 tu baada ya Simba kusawazisha bao la pili.
Wakati huo, tayari mvua kubwa ilikwishaanza kunyesha Uwanja wa Taifa na kusababisha baadhi ya mashabiki kuanza kuondoka kwa kuhofia usalama wao.
Katika mchezo huo uliokuwa wa ushindani mkali, Simba walitangulia kupata dakika ya tisa tu kupitia kwa Nahodha wake, mshambuliaji John Raphael Bocco aliyefunga kwa penalti baada ya mchezaji wa Al Masry, Mohamed Koffi kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Bao hilo halikudumu sana, kwani Ahmed Goma aliisawazishia Al Masry inayofundishwa na gwiji wa Misri, Hossam Hassan dakika ya 11  kwa shuti lililomshinda kipa Aishi Manula.
Al Masry wakapata bao la pili dakika ya 26 kupitia kwa Ahmed Abdalraof ‘Shokry’ aliyefunga kwa penalti baada ya beki Mghana, James Kotei kuunawa mpira kwenye boksi.
Kipindi cha pili, kocha Mfaransa wa Simba SC, Pierre Lechantre aliwatoa Bocco, beki Yussuf Mlipili na nafasi zao kuchukuliwa na mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo na kiungo Said Ndemla waliokwenda kuongeza nguvu kikosini.
Kasi ya mchezo wa Simba iliongezeka baada ya mabadiliko hayo na wakafanikiwa kupata bao la pili kufuatia Koffi kuunawa mpira kwenye boksi Mganda, Emmanuel Okwi akaenda kufunga kwa penalti dakika ya 73.
Kikosi cha Simba SC; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, James Kotei, Yusufu Mlipili/Ndemla dk71, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Shomari Kapombe, Emmanuel Okwi, Shiza Kichuya/Laudit Mavugo na John Bocco/Mavugo dk61.
Al Masry; Ahdem Abdelwahab, Ahmed Abdalraof, Mohamed Mahmoud, Ahmed Gomaa, Islam Salem, Amir Mousa, Islam Atta, Mohamed Emam, Farid Emam, Mohamed Koffi na Mohamed Ahmed.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top