0
Image result for RAYMOND MUSSHI BABATI 
Katika kuelekea uchumi wa kati unaotegemea viwanda katika serikali ya awamu yatano inayoongozwa na Rais John Pombe Magugufuli wanawake wilayani Babati wameonyesha kuwa wanaweza hata bila kuwezeshwa baada ya kujikita katika kilimo cha Pamba ambacho hakipatikani katika wilaya nyingine Mkoani Manyara.
Kilimo cha pamba katika mkoa wa Manyara kinafanyika katika kata tarafa ya Mbugwe pekee.
Wakina mama waliojitokeza katika kilele cha sherehe za wanawake duniani zilizofanyika katika kata ya Mwada kijiji cha Mbuyu wa Mjerumani katika taarifa yao iliyopsomwa na Afisa Maendeleo ya jamii Priska wameelezea shughuli wanazozifanya na changamoto wanazokabiliana nazo.
Akizungumza   na  mamia ya wakina mama waliojitokeza kuadhimisha siku ya mwanamke duniani yaliyofanyika katika kata ya Mwada kijiji cha Mbuyu wa mjerumani Mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi ameahidi kuwapatia mitaji na mikopo wanawake  wanaojishughulisha na ujasiaria mali katika wilaya yake.
Awali mkuu wa wilaya Mushi alitembelea mashamba ya vikundi vya wakina mama wa Mwada wanaojishughulisha na kilimo cha Pamba ambapo aliwahidi kuwa serikali itawatafutia ardhi ili waweze kuendeleza kilimo hicho cha Pamba.
Kauli mbiu ya wiki ya wanawake mwaka huu kitaifa'KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA TUIMARISHE USAWA WA KIJINSIA NA UWEZESHAJI WANAWAKE VIJIJNI.'

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top