0

Mfanyabiashara mmoja mjini Mbulu, Abie Tara amejitolea kuwasaidia vijana kuepika matumizi ya pombe kwa kuanzisha ligi ya mpira wa miguu.

Wakizungumzia michuno hiyo wakazi na viongozi wa timu wameelezea ligi hiyo ambapo leo Sanu Baray ilimenyana na Bargish katika hatua ya nusu fainali.

Mchezo wa leo ulikuwa wa kusisimua timu zote zikionyeshana ubabe dakika 90 za mchezo.
Ilimlazimu mwamuzi kuongeza dakika 30 lakini bado hali ilikuwa tete hivyo kuwapeleka katika matuta.


Sanu baray [Chama cha wana] ilipata penati 1 kati ya tano ilizopata huku Bargish akipenya katika hatua ya Nusu fainali kwa kupata penati 5.

Kocha wa  Bargish Emmanuel Bayo  alisema licha ya wapinzani wao kutamba kwa mipira mingi ya kichwa lakini Ubingwa unakwenda kwao.

Sasa Bargish alieingia leo katika hatua ya Fainali anakutana na madereva Boda boda kutoka kijiwe cha Manji.

Mmoja kati ya mashabiki wa Sanu Baray Mama Ante ametupa lawama zake kwa waamuzi wa mchezo huo akieleza kuwa wamebebwa baada ya wapinzani kuwafanyia madhambi eneo la penati na mwamuzi wa kati kupotezea adhabu hiyo ambayo ilikuwa ni penati.
 


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top