0
Mwenyekiti wa umoja wa vijana chama cha Mapinduzi UVCCM Babati vijijni Stanley Dismas Charles amewataka vijana kujiunga katika vikundi vya ujasiriamamali ili waweze kunufaika na asilimia 4 zinazotolewa na Halmashuri zote hapa nchini.

Ameyazungumza hayo alipowatembelea vijana wa kata ya Magugu ikiwa ni moja kati ya ziara zake za kikazi na kutoa shukrani kwa wana Ccm waliomchagua.
Aidha Mwenyekiti huyo amesema atahakikisha anazifuatilia  taasisi
na makampuni yanayotoa ajira kwa vijana na kuangalia kama kweli wanapatiwa stahiki zao kulingana na kazi wanazozifanya akisema ‘yapo makampuni yanawafanyisha vijana kazi zaidi ya masaa 8 huku wakilipwa pesa kidogo’.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top