0
Image result for CHADEMAWakazi wa mtaa wa mruki mjini Babati wameuondoa madarakani uongozi mzima wa serikali ya mtaa kwa madai kuwa wameshindwa kuwasimamia kikamilifu huku tuhma nyingi zikienda kwa mwenyekiti Wilson Mtatiro.
Ni wale waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka 2014.
Hayo yamefikiwa jana mei 22 katika mkutano uliofanyika katika mtaa huo uliopo kata ya Maisaka uliosimamiwa na katibu tarafa wilaya ya Babati kwa niaba ya Mkuu wa wilaya Mhandisi Raymond Mushi, ambapo wananchi hao walikubaliana kupiga kura za aina mbili,Waondoke au Wabaki,kura zaidi ya 130 zilisema Waondoke na 37 zilisema wabaki.
Baadhi ya tuhuma zilizotajwa na wananchi hao dhidi ya mwenyekiti wao nai pamoja na Ukataji wa miti na kuuza,kuuzia kokoto wakazi wa mtaa,kuuza ardhi ,uongozi kukosa utetezi kwa wananchi wake na ubinafsi.
Akijibu tuhuma hizo Mwenyekiti Wilson Peter Mtatiro amesema ‘licha ya kujitetea mbele ya wananchi hao lakini wameamua kuniondoa’ila mimi sina shida,kwanza nimetumia fedha zangu nyingi sana tangu niingie nkwenye System ya Serikali,hata mimi nilichoka,nitaendelea kufanya biashara zangu.
Erick Lema   mjumbe wa kamati ya mtaa aliejiuzulu kabla ya maamuzi ya wananchi yeye anasema hata katika mikutano mwenyekiti hataki kusikiliza hoja za wenzake hali iyokuwa ikizua mtafaruku na hata kutaka kupigana.
Diwani wa Viti maalum[ CHADEMA] Babati mjini Plaksidia Claudi  amesema kuwa kilichofanyika  cha kuwqaondoa madarakani viongozi hao ni uonevu mkubwa na kwamba ni wa kupangwa.
Wananchi wamesema kuwa wamechoshwa na tabia za Mwenyekiti huyo kwa muda mrefu kwa vitendo vyake alivyokuwa akivifanya ikiwemo dhuluma.
“Huu uongozi kupitia mwenyekiti umekuwa ni wa dhulma,mimi mwenyewe nayeongea hapa kanidhulumu elfu hamsini na tano niliyotumia nguvu zangu kuchimba mashimo ya nguzo za umeme wa Rea,nilivyofuata pesa zangu akanijibu nionyeshe tulipoandikishana kama unanidai” Alizungumza kwa uchungu Kijana Hasan Abdulmarik.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top