0


Imeandikwa Na John Walter

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis  Mwinjuma, Oktoba 10,2024 Jijini Dar es Salaam  ameonesha rasmi muonekano wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) mbele ya Waandishi wa Habari.

Akizungumza na wanahabari hao, Mhe. Mwinjuma amesisitiza dhamira ya dhati ya Serikali katika kuimarisha viwango vya tuzo hizo, ambapo mwaka huu zitatolewa Jumamosi, tarehe 19 Oktoba 2024, katika ukumbi wa The Dome Masaki.

"Sisi wasaidizi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tunaona mapenzi ya dhati  ya mama yetu kuhusiana na michezo, sanaa na utamaduni wa nchi hii,  hivyo hatuwezi kufanya vitu chini ya kiwango, ndio maana tuzo hizi zilikuwa zinaendelea kuhakikiwa" amesema Mhe. Mwinjuma.

Kwa upande wake, Katibu wa Baraza la Sanaa la Taifa, Dkt. Kedmon Mapana, amefafanua namna ambavyo mwitikio wa wasanii katika tuzo hizo imekua mkubwa. 

"Mwaka huu tumepokea kazi zaidi ya 1440, ikilinganishwa na mwaka jana, katika vipengele 36 vinavyoshindaniwa," aliongeza Dkt. Mapana.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top