Kata ya Selela Monduli Mkoani Arusha inakabiliwa na tatizo la
ukosefu wa umeme kwa zidi ya wiki nne sasa na kusababisha shughuli nyingi
kukwama ikiwemo hospitali ya zahanati katika kata hiyo kushindwa kutoa huduma
kwa wagonjwa ipasavyo hali iliyowakasirisha wakazi wa Kata na kijiji cha Selela na kumtaka
diwani wao ashuhulikie hilo mara moja.
Kata ya selela jimbo la Monduli inakabiliwa na tatizo la
umeme zaidi ya mwezi sasa.
Diwani wa kata hiyo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi [CCM] Mh.Casbeth Meena amezungumza na kipindi hiki
na kueleza kuwa amewasiliana na Tanesco makao makuu jijini Arusha na mpaka sasa
hakuna dalili zozote za kutatuliwa kwa tatizo hilo na kueleza kuwa watalishtaki
shirika la umeme kwa kuwakosesha wananchi wa Kata na kijiji cha Selela huduma
hiyo huku wakiwa tayari wameshalipia.
Diwani Meena amesema kwamba amepanga kulishtaki shirika la
umeme [TANESCO] endapo watashindwa kulitatua tatizo hilo mapema.cue Diwani
Diwani huyo amesema kuwa tangu Transfoma iliyokuwa imefungwa
kwenye kata hiyo iungue mpaka leo hakuna
kilichoendelea.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa ramani ya kijiji inaonyesha
kuwa kijiji kizima kingepata umeme pamoja na shule ya ya Sekondari lakini shule
hiyo ya Kata haina umeme na wanafunzi wanatumia sola kusomea.
Kipindi cha nyuma shule ya kata hiyo ilikuwa ikitumia taa
katika kujisomea.
Meena anaeleza kuwa kwa kukosekana kwa umeme unasababisha
shuguli nyingi za kijamii kukwama kama vile mashine za kusaga,wanaojishughulisha
na kuchomelea [welding] Saloon na kushindikana kufanyika kwa vipimo muhimu
katika zahanati ya kata.
Amesema kuwa atawasiliana na waziri mwenye dhamana wa
nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo ili amweleze malalamiko hayo
yaliyopo katika kata yake.
kuipata sauti ya diwani bonyeza hapa. http://www.audiomack.com/song/stove-iron/casbeth-meena
Post a Comment
karibu kwa maoni