Serikali
imetoa ufafanuzi kuhusu kukataza mikutano yote ya ndani na nje ya kisiasa mpaka pale watakairuhusu tena na
kusema kwamba inatokana na sababu za kiupelelezi zinazoendelea na
zitakapokamilika mikutano hiyo itaendelea.
Waziri wa
katiba na sheria Dk. Harrison Mwakyembe ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na
mwandishi wa habari baada ya kutoka kwenye hafla ya kuwaaga askari waliouawa
juzi wakiwa wanajiandaa kutoka kazini iliyofanyika Kilwa Road akiiwakilisha
wizara yake.
Kuhusu rais
Magufuli kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na kuwahimiza watu kufanya kazi
kwa ustawi wan chi,mwakyembe ambaye ni waziri mwenye dhamana ya katiba na
sheria anasema kuwa rais hajapiga marufuku siasa alichokifanya ni kudhibiti
uendeshaji huria/holela wa siasa nje ya maeneo yetu ya uchaguzi na ameafanya
hivyo kuepusha shari.
Amewataka
watanzania waiamini serikalia yao ya awamu ya tano inayosimamaiwa na RaisDk.Joseph
Magufuli kwani anayo nia njema sana kwa kuwa ameweka mbele maslahi ya taifa
hili na maslahi ya mnyonge bila kujali chama chochote.
“Hata sisi
wasaidizi wake anakwenda mbali kiasi kwamba mpaka tunasema Mungu wangu wee
hajifikirii hata yeye mwenyewe”.
Amesema kuwa
waliopanga kufanya maandamano ya UKUTA septemba mosi ni kujitafutia matatizo
yasiyo na maana akieleza kwamba dhamira yaserikali ni njema,Maandamano hayana
tija,kama kuna sera unaona haijakaa vizuri milango haijafungwa ipo wazi na rais
hajibiwi kupitia vyombo vya habari wala
maandamano bali upo utaratibu.
Mwakyembe
amehusisha tukio hilo la mauaji ya askari hao wanne na visa vya kisiasa.”Sasa kufuatia tukio hilo
baya ambalo ukiangalia mazingira yake yote lengo lilikuwa ni kuwaua hao polisi kwa sababu bank ilikuwepo karibu
lakini hawakupora pesa na kupora
silaha,lakini vile vile na viashiria vingine vya kisiasa vyenye shari, jeshi letu la polisi ambalo linabeba wajibu
kisheria kulinda amani ya nchi hii limekuja na hiyo amri ya muda kutokana na
hali halisi iliyopo kwamba ebu tusitishe hata vikao hivyo vya ndani,na mimi
kama waziri wa Katiba na Sheria nasema hiyo ni amri halali na inapaswa
kuzingatiwa, kutiiwa na kila chama cha siasa bila ubaguzi’.
Post a Comment
karibu kwa maoni