Mgogoro
wa kugombea maji umesababisha watu wasiojulikana kuweka kinyesi cha
binadamu kwenye chanzo cha maji kinachotegemewa na wananchi zaidi ya
elfu 50 wa vijiji saba vya tarafa ya Leguruki wilaya ya Arumeru mkoni
Arusha kitendo kilichoibua taharuki na hofu kubwa na kusababisha kamati
ya ulinzi na usalama ya mkoa kuhamia kwa muda katika eneo hilo
kushughulikia tatizo hilo.
Baada ya kamati hiyo kuwasili katika eneo hilo viongozi wakamweleza mkuu
wa mkoa wa Arusha Bw Mrisho Gambo kilichosababisha na hatua
walizochukuwa baada ya tukio hilo.
Mhandisi wa maji wa wilaya ya Arumeru Bi Happy Mrisho amesema mgogoro ni
wa muda mrefu na ulishika kasi baada ya kuanza kwa mradi kusambaza maji
hayo kwa wananchi wa vijiji vingine,madai ambayo yamepingwa vikali na
wananchi hao.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Mrisho
Gambo akatoa maelekezo na msimamo wa serikali ambayo yaliungwa mkono na
wananchi wote na wakakubali kumaliza tofauti zao.
Post a Comment
karibu kwa maoni