0

J LO: NIMETOKEA FAMILIA MASIKINI SANA


NYOTA wa muziki nchini Marekani, Jennifer Lopez ‘J Lo’, ameweka wazi kuwa ametokea katika maisha ya kimasikini sana, ndicho kilichompa moyo wa kutaka kuwa tajiri.
Msanii huyo mwenye miaka 47, kwa sasa anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya Dola milioni 300 ambazo ni zaidi ya bilioni 654 za Kitanzania.
“Ni wazi kwamba nimetokea katika maisha ya kimasikini, labda ningetokea katika familia ya kitajiri nisingekuwa JLo mpambanaji.
“Nilikuwa navaa kiatu kimoja kwa muda mrefu, jambo ambalo sitolisahau katika maisha yangu, lakini kwa sasa nina furaha kwa kuwa nafanya ninachokitaka na ninachokipenda,” alieleza JLo

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top