Serikali imewasilisha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa na kiwango cha ukomo wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 huku ikionyesha ukomo wa bajeti kufikia shilingi trilioni 31.6 kutoka trilioni 22 za mwaka wa fedha unaoisha Juni 30, mwaka huu
Katika bajeti hiyo, fedha za maendeleo zimeongezeka kutoka trilioni 11.8 mwaka 2016/17 hadi trilioni 11.9 mwaka 2017/18 sawa asilimia 38 ya bajeti yote.
Mapendekezo hayo yamewasilishwa hii leo bungeni mjini Dodoma ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa vikao vya bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Akiwasilisha mapendekezo hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ametaja baadhi ya maeneo ya kipaumbele kuwa niujenzi wa reli ya kati, kuhuisha shirika la ndege Tanzania na shamba la kilimo na uzalishaji sukari la Mkulazi.
Aidha, Waziri Dkt. Mpango ametaja changamoto za utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/2017 hadi Februari mwaka huu kuwa ni mwamko mdogo wa kulipa kodi na hususani kuzingatia matumizi ya mashine ya kielektroniki.
Baadhi ya wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi, nje ya ukumbi wa bunge wamesema serikali imechukua jitihada kubwa katika kuhakikisha inaondokana na utegemezi kuliko kutegemea fedha kutoka nje.
Wabunge bado wanaendelea na vikao na shughuli za utekelezaji katika kamati mbalimbali hadi Aprili 2 mwaka huu kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania April 4 mwaka huu mjini Dodoma.
==>Hii ndo Ripoti kamili iliyowasilishwa leo Bungeni
==>Hii ndo Ripoti kamili iliyowasilishwa leo Bungeni
Post a Comment
karibu kwa maoni