Mradi huo umekabidhiwa kwa BAWASA na katibu tawala wilaya ya Babati Alli Mshamu kwa Niaba ya mkuu wa wilaya mbele ya wakazi wa kijiji cha Kiongozi.
Licha ya kuukabidhi mradi huo bado tatizo la maji ni kubwa katika vitongoji vya Changarawe,Kwa Kombo Misuna na Mlangarini.
Akizungumza mara baada ya kutia sahihi mkurugenzi wa BAWASA Iddy Msuya amesema kuwa watahakikisha ndani ya siku 14 wanamalizia baadhi ya vifaa vilivyobaki ili maji yawafikie wakazi wote wa kijiji cha Kiongozi.
Post a Comment
karibu kwa maoni