0
Hoteli ya kifahari yachomwa moto KenyaHaki miliki ya pichaMUKUTAN RETREAT
Image captionHoteli ya kifahari yachomwa moto Kenya
Hoteli moja ya kifahari nchini Kenya, inayomilikiwa na raia wa Italia na mwandishi wa vitabu Kuki Gallmann, imechomwa moto na watu wanaokisiwa kuwa wafugaji.
Hilo ndilo shambulizi la hivi punde katika eneo hilo linalokumbwa na ukame la Laikipia, kutoka kwa watu wanaikisiwa kuwa wafugaji ambao wanavamia mashamba ya kibinafsi wakitafuta malisho.
Hakukuwa na wageni ndani ya hoteli hiyo ya Mukutan wakati ilichomwa.
Huenda shambulizi hilo ni la kulipiza kisasi oparesheni ya polisi, ripoti zinasema.
Hoteli ya kifahari yachomwa moto KenyaHaki miliki ya pichaTHE STAR, KENYA
Image captionHoteli ya kifahari yachomwa moto Kenya
Mapema wiki hii, polisi wanaripotiwa kuwapiga risasi na kuwaua karibu ng'ombe 100 katika shamba linalomilikiwa na Bi Gallmann.
Eneo la Laikipia lenye ukubwa wa ekari 10,000, mraba ndiko wazungu humiliki mashamba makubwa.
Hali ya usalama imedhoofika miezi ya hivi karibuni huku wafugaji waliojihami wakitafua malisho kwa mifugo wao.
Hoteli ya kifahari yachomwa moto Kenya
Image captionHoteli ya kifahari yachomwa moto Kenya

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top