0
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Dakta Joel Bendera
Mwekezaji wa shamba lililokuwa na mgogoro na wananchi wa kijiji cha SHAURIMOYO wilaya ya Babati mkoani Manyara kwa zaidi ya miaka kumi ameamua kurejesha shamba hilo kwa serikali ili kumaliza mgogoro na wananchi.

Mwekezaji huyo Kampuni ya Republic Body Builders .Ltd amerejesha shamba la ukubwa wa ekari 1,098 kutokana na mgogoro baina yake na wananchi uliosababisha uharibifu wa mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tatu.

Akikabidhi hati kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mkurugenzi wa shamba hilo Parvinder Singh Nyotta amesema ameamua kufanya hivyo ili kumaliza mgogoro na wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Manyara Dakta Joel Bendera amesema hatua ya mwekezaji huyo kutoa shamba kwa wananchi imemaliza mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi.

Wakati wa mgogoro huo wananchi walivamia mashamba na kuteketeza mali za mwekezaji huyo na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni tatu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top