PAMOJA na ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana, Nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba mshambuliaji Thomas Emmanuel Ulimwengu ni muhimu katika timu hiyo.
Taifa Stars jana iliichapa Botswana 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Samatta akifunga mabao yote, moja kila kipindi.
Lakini baada ya mchezo huo, mshambuliaji huyo wa KRC Genk ya Ubelgiji akasema ameliona pengo la Ulimwengu kwenye mchezo huo wa kwanza chini ya kocha Salum Mayanga aliyerithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa.
“Kitu kingine ni kwamba mimeliona pengo la Ulimwengu, huyu mtu ni muhimu ambaye tumemkosa kwenye mchezo huu kwa sababu ni majeruhi, lakini anahitajika sana kwenye timu,”alisema Samatta kuhusu mchezaji mwenzake huyo wa zamani wa TP Mazembe ya DRC.
Kwa sasa Ulimwengu anachezea AFC Eskilstuna ya Ligi Kuu ya Sweden na ameshindwa kujiunga na Taifa Stars kwa sababu yuko chini ya uangalizi wa Dakatari nchini humo.
Post a Comment
karibu kwa maoni