Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mpaka jana joini zilikuwa bado zimefungwa kutokana na ofisa mmoja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoziona funguo za ofisi hizo alipoziweka.
Ofisi za TFF zilifungwa Jumatano ya wiki hii kufuatia limbikizo la deni ambalo ni zaidi ya shilingi bilioni moja la tangu mwaka 2010 ikiwa ni deni la kodi la ujio wa timu ya Brazil, kodi ya mshahara wa aliyekuwa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Marcio Maximo pamoja na deni la mwaka jana la mechi ya Yanga na TP Mazembe ambao mashabiki waliingia bure.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa, hadi kufikia jana mchana ofisi hizo hazikuwa zimefunguliwa kutokana na baadhi ya mambo kutokamilika ikiwa ni pamoja na kutoonekana kwa funguo za ofisi hizo.
“Jana (juzi) viongozi wa TFF walikutana na TRA kujadiliana suala hilo na kufikia muafaka ambapo kiasi cha fedha Sh milioni 300 kililipwa ili kuweza kufungua ofisi hizo lakini ilishindikana kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo.
“Tumewasiliana nao leo lakini muhusika ambaye anatakiwa kufungua ofisi amesahau alipoziweka funguo,” alisema Lucas.
Post a Comment
karibu kwa maoni