Wanasayansi wanasema kuwa wamepiga hatua kubwa katika uzalishaji wa damu yenye seli nyekundu kwa wingi itakayotumiwa kuwasaidia wagonjwa.
Seli yekundu hutengezwa katika maabara lakini tatizo ni kiwango kinachohitajika.
Kundi moja la wanasayansi katika chuo kikuu cha Bristol pamoja na idara ya damu na upandikizaji limetengeza mbinu ya kuzalisha kiwango kikubwa cha damu.
Damu hiyo ya maabara itakuwa bei ya juu ikilinganishwa na damu ya kawaida.
Kwa hivyo itatumiwa miongoni mwa watu wasio na aina ya damu.
Mfumo wa zamani ulishirikisha kutumia kiini shina kinachotengeza seli nyekundu za damu katika mwili na kuzibembeleza kuzalisha seli kama hizo katika maabara.
Hatahivyo kila seli huchoka haraka na kushindwa kuzalisha zaidi ya seli nyekundu 50,000.
Mbinu iliotengezwa na kundi hilo la wanasayansi wa Bristol inalenga kuzishika seli shina mapema wakati zinapokuwa kwa wingi.
Hatua hiyo hujulikana kama kuzifanya seli hizo kuishi milele.
Wakati watafiti wanapozipata aina hizo za seli huzifanya kuwa seli nyekundu.
Daktari Jay Frayne mmoja ya watafiti wa kundi hilo alisema: Tumeonyesha uwezo wetu wa kuzalisha seli nyekundu zinazoweza kutumiwa katika hospitali.
Tumezalisha nyingi. Damu katika mfereji?
Watafiti hao wana uwezo wa kibaiolojia kuzalisha seli nyekundu nyingi lakini wanahitaji mfumo wa kiteknologia ili kuzalisha seli nyingi zaidi.
Ni sawa na tofauti ya kuzalisha pombe nyumbani na kutengengeza kwa wingi kiwandani
Post a Comment
karibu kwa maoni