Mkuu wa Mkoa wa MANYARA Dakta JOEL BENDERA ametoa wiki mbili kwa Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya HANANG’ kupitia na kuhakiki madai ya walimu na kuwasilisha kwake kwa hatua zaidi.
Dakta BENDERA ametoa agizo hilo kufuatia kauli za baadhi ya walimu wa wilaya hiyo kuwa kushuka kwa elimu wilayani humo kunatokana na baadhi ya walimu kukosa ari ya kufanyakazi kwa moyo.
Bila woga wala kumung’unya maneno walimu hao wamemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa baadhi yao hawana ari ya kufundisha kutokana na serikali kutowajali kwa madai yao.
Amesema kisaikolojia amebaini kuwa baadhi ya walimu hao wana mgomo baridi.

Post a Comment
karibu kwa maoni