Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
amewasili Zanzibar akitokea Mjini Amman Nchini Jordan kuhudhuria Jukwaa
la Dunia la Uchumi World Economy Forum – WCF} la Siku Tatu
litakalohudhuriwa na zaidi ya Wajumbe 2,000 kutoka Nchi 58 Duniani.
Balozi Seif alimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwenye Jukwaa hilo la Kanda ya
Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika lililoshirikisha Viongozi
Wakuu wa Nchi, Wafanyabiashara,wamiliki wa Makampunni ya Kimataifa,
Wawakilishi wa Taasisi za Kiraia, Mashirikia ya Kimataifa, Wana Habari
pamoja naVijana wapatao 2,000.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokewa na baadhi ya Mawaziri,
Watendaji Wakuu wa Serikali pamoja naViongozi wa Kisiasa.
Katika Mkutano huo wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Balozi
Seif aliongozana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar
Balozi Amina Salum Ali, pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili
wa
Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed.
Katika Mkutano huo wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Balozi Seif na Ujumbe
wake alishiriki Washa ya Utalii iliyojikita zaidi katika masuala ya
Kujenga Uchumi kwa Mataifa yaMashariki ya Kati na yale ya Kanda ya
Afrika ili kuona njia gani
zinaweza kutoa fursa za ajira kwa Vijana kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa
Mkutano huo wa Jukwaa la Uchumi Duniani ulifunguliwa na Kiongozi wa
Jordan Mfalme wa Pili Abdullah Bin Al-Hussein kwenye Ukumbi wa
Kimataifa wa King Hussein Bin Talal katika Bahari Nyeusi.
Jukwaa la Uchumi la Dunia { World Economy Fforum – WCF}
limeasisiwa Mwaka 1971 chini ya Muanzilishi na Mwenyekiti wake Profesa
Klaus Schwab huko Davos, Switzerland. Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na baadhi
ya Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Serikali mara alipowasili kwenye
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume akitokea Nchini Jordan
kushiriki Mkutanowa Jukwaa la Dunia la Uchumi akimuwakilisha Rais wa
Jamuhuri ya Mauungano wa Tanzanmia Dr. John Pombe Magufuli. Balozi
Seif Kushoto akibadilishana Mawazo na Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar katika chumba cha Watu Mashuhuri {VIP} Kongwe.
Post a Comment
karibu kwa maoni