0
Responsive image
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick

Serikali Mkoani Kilimanjaro imekifunga kiwanda bubu cha kuzalisha pombe ya kienyeji aina ya Banana Wine kilichopo Wilayani Moshi kutokana na kutokuwa na vibali halili vya uendeshaji wa biashara hiyo.
Akitoa agizo la kufungwa kwa kiwanda hicho Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick pia ameliagiza Jeshi la Polisi kumsaka mmiliki wa kiwanda hicho Gibson Lyimo ili achukuliwe hatua za kisheria.
Meck Sadick amesema mbali na kutokuwa na kibali mazingira ya kiwanda hicho hayaridhishi hivyo kuhatarisha usalama wa afya za watumiaji wa kinywaji hicho.
Nao baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo wamesema  pombe za kienyeji zimekuwa zikiathiri afya za vijana katika maeneo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top