Mahakama ya Sharia katika mkoa wa Aceh nchini Indonesia, imewahukumu wanaume wawili kuchapwa viboko hadharani kwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
Wanaume hao walipatikana na hatia ya kukiuka sheria kali za kiislamu na hivyo watachapwa viboko 85 kila mmoja.
Wawili hao wenye umri wa miaka 20 na 23 walipatikana wakifanya mapenzi kitandani mwezi Machi.
Mapenzi ya jinsia moja si haramu kwenye taifa hilo lenye waislamu wengi na ndiyo hukumu ya kwanza ya aina hiyo kutolewa.
Licha ya hukumu hiyo kukosa kutoa adhabu ya viboko vingi zaidi ambavyo ni 100, hukumu yenyewe ilikuwa nzito kuliko ya viboko 80 iliiyoombwa na wakuu wa mashtaka.
Hukumu za kuchapwa viboko zimetolewa kwa makosa ya kucheza kamari na unywaji pombe.
Hata hivyo hukumu hiyo imekosolewa na watesi wa haki za binadamu na wanaharakati.
Post a Comment
karibu kwa maoni