BARAZA la Madiwani la halmashauri ya mji wa Babati kupitia Mkurugenzi wa halmashauri hiyo limewafukuza kazi watumishi wane (4) wa Serikali wa wilaya hiyo kwa makossa mbalimbali akiwemo mwalimu mmoja wa shule ya sekondari.
Akisoma taarifa ya maamuzi hayo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mohamedi Kibiki alisema kuwa halmashauri imefikia uamuzi huo kutokana na watumishi hao kukiuka maadili ya kazi kwa kutoroka kazini muda wa kazi na mmoja kugushi cheti cha kidato cha nne (4).
Kibiki aliwataja watumishi hao kuwa ni Asha Hamis Abadallah aliyekuwa mtendaji wa mtaa wa Oysterbay, kata ya Babati aaliyegushi cheti, Dawi L. Sumaye mtendaji wa mtaa wa Wang’boo kata ya Bonga ambaye hakuweza kufika kazini siku tano (5) mfululizo bila taarifa.
Wengine ni Josephat Kimario Afisa mifugo kata ya Babati mwenye ngazi ya daraja ‘A’ na Mwalimu Ephraim J. Yaawo, mwalimu wa leseni wa shule ya sekondari Kwaang’w wote wakiwa na kosa la kutofika kazini Zaidi ya siku tano (5) mfululizo bila taarifa.
Akizungumzia uamuzi huo Mwenyekiti Kibiki alieleza kwamba watumishi hao wamekosa nidhamu sehemu zao za kazi na kwamba nidhamu inahitajika kwa watumishi ili kuepuka misukomisuko kama hiyo na mingine ndani ya maeneo yao ya kazi.
“Hakuna anayependa kumfukuza mtu kazi ila ni sheria ndiyo inatubana, maamuzi haya ni magumu sana lakini hayuna jinsi kama kamati tumekaa na tumeazimia kwa vifungu vya sheria, kumfukuza mtu kazi ni kumpa wakati mgumu sana kwani anakwenda kuanza maisha mengine ambayo hakuyategemea”, alisema Kibiki.
Aidha aliwaasa watumishi kuwa makini katika maeneo yao ya kazi na ajira zao kwa ujumla na kueleza kwamba kuwakosesha wananchi huduma za kijamii kunasababisha migongano na migogoro isiyo ya lazima.
“Niwaombeni sana watumishi mlio kwenye ajira kwasasa muwe makini hasa katika maeneo yenu ya kazi, ogopeni sana kutuhumiwa na wananchi ili kuepuka madhara kama haya yaliyowakuta wenzenu”, alisisitiza.

Post a Comment
karibu kwa maoni