0
Tembo wakiwa wamejificha kwenye vichaka ndani ya eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo. Kwa mujibu wa taarifa za Wahifadhi wa Wanyamapori inaelezwa kuwa sehemu ya eneo hilo litakuwa ni njia ya tembo (maeneo ya mapito ya wanyamapori) ambayo ilipitika kwa miaka mingi iliyopita na kwamba tembo wana kumbukumbu hata kama walipita njia hiyo kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita. Imeelezwa kuwa njia hiyo ya mapito ya wanyamapori itakua ilitumiwa na wanyamapori kuhama eneo moja hadi jengine ikiwemo maeneo ya hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Ruaha, Serengeti, Pori Tengefu la Rugwa na maeneo mengine ya hifadhi na kwamba maeneo hayo mengi kwa miaka ya hivi karibuni yameshaingiliwa na shughuli za kibinadamu ambazo hazisababishi tembo hao kusahau njia hizo au kutokuzitumia tena.
Tembo hao wakiwa ndani ya eneo chuo kikuu hicho cha Dodoma leo. Hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa kusababishwa na tembo hao na taratibu za kuwarudisha kwenye maeneo yao ya hifadhi zimeshaanza kuchukuliwa na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo Askari wa Wanyamapori wamefanya zoezi la kuwafukuza kuwarudisha kwenye maeneo yao ya hifadhi.
Prof. Julius Nyahongo wa Chuo Kikuu cha Dodoma akitoa somo kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma namna ya kuchukua tahadhari juu ya ugeni wa tembo hao chuoni hapo. Aliwaeleza wanafunzi hao kuwa mazingira ya chuoni hapo yataendelea kuwa salama kwakuwa tembo hao wapo katika njia yao ya mapito na pengine kumewahi kukucha kabla ya wao kufika mwisho wa safari yao, hivyo kwa msaada wa askari wa wanyamapori ambao wamewasili chuoni hapo itasaidia kuwaondoa tembo hao waweze kuendelea na safari yao hadi kwenye maeneo ya hifadhi.
Wanafunzi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dodoma walikusanyika wakiwa na shauku ya kuwaona tembo hao.
Nakumbuka mwaka 2012 katika mji wa Mbulu mkoa wa Manyara tembo wanne walipita kati kati ya mji wataalamu wakidai kuwa ni eneo ambalo walishapitaga miaka ya nyuma na kwamba ni lazima wapite katika maeneo hayo hata kama ni miaka mingi imekwishapita
Wakazi wa mjini Mbulu na vijiji vyake walipata hofu kubwa huku wakijitokeza kwa wingi kuwatizama tembo hao waliokuwa wakipita katika maeneo hayo na kula mbahazi.
Baadaye walifika askari wa misitu kutoka hifadhi ya Manyara na kuwarudisha msituni japo ilichukua muda mrefu kuweza kuwaondosh Katika mazingira ya binadamu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top