Sarah Bundala (55) amejiua kwa
kujinyonga kutokana na kutokua na uwezo wa kutorejesha pesa za mkopo
alizo mdhamini rafiki yake ambae ametoroka.
Sarah akiwa ni mkaazi wa mtaa wa
Tambukareli kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga.
Akisimulia kuhusu tukio hilo rafiki
yake Mariam Mgaya, alisema kuwa majira ya saa nane mchana siku ya tukio
alimuita ili amsindikize wakatafute pesa za kukopa, ili akarejeshe marejesho
lakini walivyozunguka na kukosa ndipo akamshauri ampigie simu mume wake
amsaidie kiasi hicho cha pesa anachohitaji akagoma kufanya hivyo.
Alisema baada ya kushauriana
wapi watapata pesa na kukosa majibu, marehemu alimwambia anataka kwenda
nyumbani kulala kwanza na ikifika majira ya saa 10 arudi kumuona na hata watu
wakimuuliza yuko wapi awaambie amelala nyumbani kwake asiwafiche na ilipofika
muda huo akapokea taarifa rafiki yake amejinyonga.
Akizungumzia tukio hilo mume wa
marehemu Laurent Mabina, alisema wakati akiwa bado kazini majira ya saa 9
mchana alipigiwa Simu na mke wake akimuomba Shilingi 40,000/- akamjibu kuwa
anarejea nyumbani muda huo na akifika wataangalia cha kufanya lakini alipofika
akakuta mkewe amejinyonga.
“Mke wangu alishawahi kukopa fedha
akashindwa kulipa nikalazimika kulipa na kumuonya kwamba asijiingize tena
kwenye masuala ya mikopo,huenda sababu ya mke wangu kujinyonga ni ile hofu kuwa
nikirudi nyumbani nitakuja kugombana naye sababu nilishamkataza mambo ya
mikopo” alisema Mabina.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani
Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro alithibitisha kutokea kwa tukio hilo
lililotokea jana Ijumaa Julai 14,2017.
Post a Comment
karibu kwa maoni