Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imetoa ndege kwaajili ya kusafirisha mwili wa mke wa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kuelekea Kyela.
Majaliwa ameyasema hayo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri huyo kwaajili ya kumpa pole na kumfariji kwa kipindi hiki kigumu alichoondokewa na mke wake marehemu Linah George Mwakyembe.
“Serikali inakupa pole sana wewe ndugu na wanafamilia kwa ujumla kwa kuondokewa na mke wako Linah, nawaomba muwe wavumilivu katika kipindi hiki kigumu na Serikali imetoa ndege ambayo itabeba mwili wa marehemu kuupeleka nyumbani Kyela,”amesema Majaliwa.
Hata hivyo,
mwili wa marehemu Linah unatarajiwa kuagwa siku ya jumanne jijini Dar es salaam
tayari kwaajili ya kusafirishwa kupelekwa Kyela kwaajili ya mazishi hapo siku
yaju jumatano.
Post a Comment
karibu kwa maoni