0

 August 9 2017 ulifanyika mkutano na Waandishi wa habari ukimuhusisha Mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Ruge Mutahaba, RC wa DSM Paul Makonda na Jukwaa la Wahariri kuhusu ishu ya kufungiwa kwa habari za Mkuu wa mkoa Paul Makonda.

Baada ya mkutano huo na mengine yaliyojadiliwa na kauli zilizotolewa ikiwemo ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kusema hawezi kuomba radhi, Ruge Mutahaba amehojiwa na vyombo vya habari baada tu ya mkutano huo kuisha na kueleza msimamo wa CLOUDS.

“Baada ya jambo la leo msimamo wa CLOUDS MEDIA GROUP ni uleule tuliokua nao toka siku ya jumamosi baada ya kupatanishwa na Mh. Rais, siku ile alivyotupatanisha sisi kama Watanzania hatukua na budi zaidi ya kukubali na kurudi kwenye uhusiano wa kiuweledi”
KWA UPANDE WA MAKONDA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa kamwe hawezi kuomba radhi kwa tukio lilitokea Clouds Media Group (CMG) kwa sababu hukumu iliyotolewa na Jukwaa la Wahariri ilikuwa ya upande mmoja.
Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambapo amesema hukumu hiyo ilikuwa ya upande mmoja  hivyo hilo lilikuwa ni  jambo lake yeye kumalizana na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba.
“Nimesema sitaomba msamaha kamwe, kwa suala hili, kwani kile kilichosemwa kuwa nimevamia Clouds Media sio cha kweli, tafsiri ya neno uvamizi ni kubwa sana, wala TEF hawana makosa kutoa hukumu yao kwakuwa walisikiliza upande mmoja,”amesema Makonda.
Hata hivyo, ameongeza kuwa hakuna haja ya kuendelea na malumbano yasiyokuwa na msingi wowote, kwani adhabu iliyotoka tayari ilishachukuwa ya muda mrefu hivyo ni bora ikaisha.

WANAHABARI

Mwandishi wa habari Leine Allivin kwenye ukurasa wake wa facebook ameandika haya.
Mimi Leine Allvin Mwanahabari (Kitaaluma)
Nimesikitishwa sana na tukio la leo la Jukwaa La Wahariri.
Hivi Meena kweli???????
Tunajenga Taaluma Ya Aina Gani
Leo Wahariri wenye heshima wamehaririwa

Nimejiuliza mengi sana..Baada Ya Kikao Na D A B
Wahaririwa Tafakarini Mchukue Hatua
Mtu Mzima akivuliwa Nguo Huchutama ila Leo Mmeamua Kukimbia Bila Kuchutuma (Wacha tuzomewe)
Hongera Ruge Mutahaba....
#Haririni Vyeti Vyenu Shubaaaaaaamiti
MEENA KAOMBA RADHI KWA WANA HABARI KUPITIA TWITWER

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top