Chama cha
demokrasia na Maendeleo chadema kimemtaka rais John Pombe Mgufuli kuruhusu
mikutano ya hadahara ya vyama vya siasa ili waweze kuzungumza na wananchi.
Hayo
yameelezwa na afisa oganizesheni kanda ya kasakazini Ndonde Totinan wakati
akizungumza leo katika mkutano mkuu wa chama hicho jimbo la Babati mjini ambapo
amesema tangu kupigwa kwa marufuku mikutano hiyo wameshindwa kufanya baadhi ya
mambo muhimu ikiwemo kuzungumza na wananchi na kuwaeleza mipango na mikakati
waliyonayo katika majimbo.
Naye
Mwenyekiti wa Jimbo la Babati mjini Hassana Madole amesema kuzuiwa kufanyika
kwa mikutano ya kisiasa na kuzuia katiba kufanya kazi hivyo amemuomba rais
Magufuli alegeze sharti hilo.
Chadema
jimbo la Babati mjini limefanya mkutano wake mkuu na kuwakutanisha wajumbe
katika ngazi zote ili kuweka mikakati ya kuimarisha chama chao.
Ikumbukwe
kuwa CHADEMA ndio chama kinachoongoza katika Halmashauri ya Babati mji,Mbunge
na viti vitano vya udiwani huku CCM ikiwa na viti vitano vya udiwani kati ya
kata nane zilizopo katika jimbo hilo.
Nae mmoja wa wajumbe wa chama hicho kutoka kata ya Maisaka ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa
wa Maisaka Wilson Peter Mtatiro amesema kuwa wamekuwa wakishindwa kufanya
shuguli mbalimbali za kisiasa kwa kushindwa kuzungumza na wananchi na pia
kupoteza wanachama.
Post a Comment
karibu kwa maoni