0

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala amezunguzia tukio la kuteketea kwa Moto Soko la Sido lililopo maeneo ya  Mwanjelwa jijini Mbeya.
Mkuu wa mkoa alizungumza juu ya tukio hilo  kwa kutoa pole na kuwataka wananchi wawe watulivu na kusubiri Serikali ifanye tathmini ya thamani pamoja na chanzo cha moto.
‘’Kwanza kabisa napenda kutoa pole kwa wananchi wa Mbeya hususani wafanya biashara wa Soko la Sido ambalo limeteketea majira ya  saa3 Usiku na Serikali inafanya tathmini ya thamani na chanzo cha moto ,tunawaomba wananchi wote wawe na uvumilivu mpaka hapo ambapo tutakapo toa tathmini nzima ya tukio lililotokea’’ Alisema Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala.
Moto huo ambao ulizuka ghafla majira ya saa3 usiku na kuzusha hofu kubwa kwa wakazi wa jiji la Mbeya, pamoja na watu walio kuwepo karibu na tukio hilo walionesha jitihada zao za kuuzima moto huo huku wakisaidiana na kikosi cha zima moto kwaajiri ya kupambana na moto huo ambao ulikua unawake kwa kasi kubwa.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top