0


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania kutolalamika kwa uamuzi wowote unaofanywa na serikali ya sasa, kwani una nia njema kwa mustakabali wa Taifa.
Mwigulu amewataka Watanzania kuendelea kumwombea Rais John Magufuli ambaye anadhihirisha kwa vitendo kuchukia wizi na ufisadi ili nia njema aliyonayo kwa taifa, aifikie. Akitoa salamu katika ibada ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbezi Luis, Dar es Salaam jana, Mwigulu alisema kuna uamuzi Serikali inaochukua huenda usieleweke kwa haraka lakini una lengo jema kwa taifa.
Alitoa mfano kuwa Rais Magufuli anachukia kwa vitendo rushwa na ufisadi hivyo hawezi kucheka wakati akifanya uamuzi, kwa kuwa hakuna dini yoyote inayomchekea shetani wakati wa kumkemea. “Ili nchi ipige hatua kuna mambo yalikuwa lazima yafanyike. Kuna mambo si rahisi kuyaelewa kwa haraka haraka, lakini niwasihi mwendelee kumwombea rais kwa kuwa ana nia njema.
“Mkimwombea Rais na sisi tunapata lifti humo humo na mambo yanaenda,” alisema Mwigulu. Alisema uovu ni lazima ukemewe na kutolea mfano Yesu Kristo alipoingia hekaluni na kukuta biashara inafanyika, alipindua meza na kufungulia njiwa kwa ukali na ndivyo anavyofanya Rais. “Mmeshawahi kuona shetani anakemewa kwa upole? Uovu lazima ukemewe kwa nguvu,” alisema Mwigulu.
Kuhusu kuchangia ujenzi wa kanisa hilo, Mwigulu alisema ni muhimu kuchangia ujenzi wa nyumba za ibada kwa kuwa zinapunguza uovu katika jamii. Alisema mikoa yenye nyumba nyingi za ibada, uovu nao unapungua na ikiwa watu hawatajitoa kuchangia Mungu, huruhusu wapate hasara ili ifidie uchoyo waliouonesha kumwibia Mungu. Kanisa hilo la Usharika wa Mbezi Luis linajengwa kutokana na bomoabomoa inayoendelea katika barabara ya Morogoro .

Post a Comment

karibu kwa maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top