Mwakyoma (RPC Mstaafu) alikuwa Kamanda wa Polisi pia katika mikoa ya Pwani na Mara kwa nyakati tofauti, alishinda kiti hicho kutokana na kukosa mpinzani na hivyo kupigiwa kura ya ‘Ndiyo’ na Wajumbe wote 25.
Katibu wa CCM Manispaa ya Moshi, Sixtus Mosha, amesema Mwakyoma alijitokeza peke yake kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi hiyo Agosti 3 na kisha akachaguliwa kwa kupita bila kupingwa Agosti 6, mwaka huu.
“Hakuna namna nyingine zaidi ya kuwapa ushirikiano wa kukijenga chama chetu hawa viongozi waliochaguliwa, na siyo kujenga makundi au majungu. Tunataka wawe mstari wa mbele kumuunga mkono Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk. John Magufuli kutekeleza ilani sawa sawa,”amesema Sixtus
Anasema katika chaguzi za kata zote 21 za Manispaa ya Moshi waliwataka wana CCM kutumia vyema chaguzi hizo kuwaweka madarakani viongozi ambao sit u wataendana na kasi ya Mwenyekiti wao wa taifa Rais Magufuli, bali watakaokihakikishia chama ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
Mwakyoma alikuwa RPC wa mkoa wa Kilimanjaro, kati ya mwaka 2011 hadi 2012 alipohamia mkoani hapa, akichukua nafasi ya Lukas Ng’hoboko aliyekuwa mtangulizi wake katika kiti hicho kati ya mwaka 2006 hadi 2011.
Katika uchaguzi mwingine wa nafasi kama hiyo katika Kata ya Shirimatunda, Mwenyekiti aliyekuwa akitetea nafasi yake Bonifasi Mmasy ameangushwa vibaya kwa kupata kura sufuri, baada ya Juma Mmasy kushinda kiti hicho kwa kura 24.
Nafasi nyingine za kata zilizowaniwa na kupata viongozi na wawakilishi ni katibu wa kata, katibu wa siasa na uenezi, mjumbe wa mkutano mkuu mkoa na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya.
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.