Video hiyo ambayo iliachiwa rasmi juzi pia imeendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwenye orodha ya video zote zinazotrend Tanzania na Kenya. Rekodi hii imetajwa kuvunja rekodi ya Afrika Mashariki.
Rekodi hii inafuatiwa na rekodi iliyowekwa na video ya wimbo wa Diamond akiwa na RayVanny ‘Salome’ ambayo iliangaliwa mara milioni moja ndani ya saa 48, miezi kadhaa iliyopita.
Hata hivyo, kuna kila dalili kuwa ‘Seduce Me’ ikaendelea kupata ‘views’ nyingi zaidi kutokana na jinsi inavyoendelea kuangaliwa kwa kasi. Kwa wastani, ndani ya dakika moja video hiyo kwa sasa huangaliwa zaidi ya mara 1000.
Hadi sasa ikiwa ni chini ya saa 48 imeangaliwa zaidi ya mara 1,500,000 ikivuta zaidi ya ‘comments’ 8,000.
‘Seduce Me’ ni wimbo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Ali Kiba ambaye alikuwa kimya kwa takribani mwaka mmoja.
Post a Comment
karibu kwa maoni