AIBU!
Nimeiona Barua kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuvitaka Vyama vya siasa vitoe maoni kuhusu utungwaji wa Sheria Mpya ya Vyama vya Siasa. Nilijua kwamba jambo hili lingefuata. Serikali inachukua hatua hii wakati huu ili kubariki "UJINGA" wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa siku za usoni.
Lengo kubwa kuliko yote ni kuweka kipengele kitakachoeleza kuwa "Msajili wa Vyama vya Siasa anaweza kuingilia mambo ya ndani ya vyama vya siasa na kwamba uamuzi wake utakuwa wa mwisho."
Yaani, kumlinda mtu mmoja, LIPUMBA, ili aimalize CUF, kunafanya hadi sheria zibadilishwe haraka ili AIBU zinazofanywa na Msajili zilindwe.
Tumewahi kuwaeleza huko nyuma mara kadhaa, kwamba Mahakama Kuu imewahi kutamka bayana katika maamuzi mbalimbali, kuwa "Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya vikao vya vyama vya siasa kwa njia yoyote ile."
CUF ilipoanza kupigwa vita na LIPUMBA akiwa mtumiwaji mkuu, wapo watu walitucheka. Tuliwaambia shambulio dhidi ya CUF ni shambulio dhidi ya demokrasia.
Tusubiri wapitishe hiyo sheria yao, uone vyama vitakavyoporwa uhuru wa ndani. Na huko ndiko CCM inapenda twende, maana yanyewe haiwezi kuguswa na Msajili ambaye obvious anateuliwa na Mwenyekiti wa CCM.
#NOTE; Hata ikitungwa sheria hii hivi sasa, mashauri ya CUF yaliyoko mahakamani yatatumia viwango vya mamlaka ya msajili yaliyotajwa kwenye Sheria Namba 5 ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 (sheria ya sasa).
#Kama mngekuwa na akili mngetunga sheria ya kuhimiza ujenzi wa kiwanda kimoja kikubwa kila kata. Lakini mko likizo!
Mtatiro J
Post a Comment
karibu kwa maoni