Watu
11 wakiwemo madiwani wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya IKungi mkoani
Singida wamekamatwa wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kuishinikiza
Serikali kutoa tamko kuhusu kuvamiwa na kupigwa risasi mwanasheria mkuu
wa Chadema, Tundu Lissu.
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu amesema watu hao wamekamatwa na
polisi jana Ijumaa mchana wakiwa na mabango katikati ya mji wa Ikungi,
wakiwa kwenye harakati za kuhamasisha maandamano.
“Walitaka
kufanya maandamano, tuliwawahi kabla hawajaanza, miongoni mwao wapo
waliotokea Arusha na Dodoma, kwa hiyo wamekamatwa kwa ajili ya mahojiano
zaidi," amesema Mtaturu.
Amesema
tukio la Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki kupigwa risasi
halijatokea Singida, hivyo hawataruhusu maandamano ya aina yoyote
yanayoweza kuhatarisha amani.
Post a Comment
karibu kwa maoni