0
Aliyekuwa mwenyekiti wa vijana wa CHADEMA kata ya Monduli Mjini mkoani Arusha Haji Adinani Mganga amezikwa na mamia ya watu huku akiacha Simanzi na vilio kwa wengi.

Haji Athumani alipata ajali siku ya ijumaa septemba 7 mwaka huu alipokuwa akivuka bara bara wakati anaendesha Piki piki yake[ Boda boda] Monduli mjini ndipo lilipotokea gari na kugonga hali iliyomsababishia kupata majeraha katika maeneo mbalimbali ya mwili wake na kukimbizwa katika hospitali ya Luteheran Selian jijini Arusha.

Hata hivyo jitihada za madaktari hazikuzaa matunda kwani walijaribu kila namna ya kuokoa maisha yake lakini ilishindikana na ilipofika siku ya jumamosi septemba 9 majira ya saa tano usiku wakati bado madaktari wanasumbuka kuokoa uhai wake Haji alikata kauli na kupoteza Maisha,kwa mujibu wa Alex Habibu ndugu aliekuwa akimuuguza mpaka anakutwa na mauti.

 Haji amezikwa nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani wilayani Monduli mkoani Arusha . Marehemu enzi za uhai wake aliishi na watu vizuri na kucheka nao muda wote huku akimtumikia Mungu na kujitolea pale ilipohitajika afanye hivyo.

 Kwa mujibu wa Kiongozi wa dini ya Uislamu Monduli Mwalimu Swalehe alimtaja marehemu kama mcha Mungu na mtu wa kujitolea na pia aliahidi kutoa mchango wa ujenzi wa msikiti unaoendelea katika mtaa wa mlimani .

 Chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema kimeeleza kusikitishwa na kifo cha Haji na kueleza kuwa kimepoteza kijana mchapakazi na kiongozi mwenye kujua watu.

Katika hatua nyingine viongozi wa dini,siasa na watu wengine walijitolea kumchangia mtoto pesa kwa kumfungulia akaunti katika bank kwa ajili ya kumwezesha kusoma ambapo zilipatikana zaidi ya shilingi milioni mbili.

 Marehemu Haji Adinani Mganga amefariki akiwa na umri wa  miaka 28, ameacha mke mmoja na mtoto mmoja.  

Inna lillahi wa inna ilaihi rajiun (To Allah we belong and to Him is our return). . Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema Peponi Amin.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top