0



Idd el Hajj (pia: eid el hajj) ni sikukuu ya Uislamu wakati wa mwezi wa Dhul Hijjah ambao ni mwezi wa Hajj.
Kati ya Waislamu duniani sikukuu hii hujulikana kwa majina mbalimbali ambayo hutafsiriwa pia kwa lugha mbalimbali kama vile:
·  dd-al-Adhha (kar. عيد الأضح) yaani sikukuu ya sadaka
·  Idd-al-Qorban (kar. عید قربان) sikukuu ya sadaka (kwa kutumia neno tofauti ya "sadaka" katika Qurani); Kituruki: Kurban Bayramı; Kikurdi "Cejna Kûrbanê" ;
·  Idd-al-Kabir (عيد الكبير) au "sikukuu kubwa"; "Bari Eid" huko Uhindi na Pakistan; jina hili hutumiwa kwa sababu kati ya sikukuu mbili zinazoamriwa katika Qurani hii ni sikukuu kubwa zaidi.
Idd husheherekewa kama kumbukumbu ya sadaka ya Ibrahimu (Abrahamu) ambaye kufuatana na taarifa za Biblia na za Qurani alikuwa tayari ya kumchinja mwanawe kama sadaka kwa Mungu. Lakini Mungu alimzuia asimchinje akampatia kondoo badala yake. Habari zake kati Qurani ziko sura al-Hajj aya 37, katika Biblia Mwanzo 22.
Sherehe huanza na sala ya idd katika msikiti. Mara nyingi hufuatwa na baraza au mkutano wa Waislamu. Katika nchi nyingu huwa na kawaida kutembelea pia makaburi ya marehemu.
Kila Mwislamu mwenye uwezo hupaswa kumchinja mnyama wa sadaka siku hiyo mara nyingi kondoo lakini kuna pia sadaka za mbuzi, ng'ombe au ngamia kufuatana na uwezo na kawaida ya nchi.
Sehemu ya nyama ya sadaka hizo hugawiwa kwa maskini wasio na uwezo. Mengine hutumiwa kwa karamu ya familia.
KWA HISANI YA WIKIPEDIA.
 

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top