0
Waziri wa Fedha na Mipango nchini Mhe Philip Mpango amesema kitendo cha watu kuhujumu uchumi wa nchi na rasilimali za taifa, ni kitendo cha kinyama na hakivumiliki, na pia ni ufisadi wa hali ya juu.

Akizungumza kwenye makabidhiano ya ripoti ya madini yaliyozuiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Nyerere jijini Dar es salaam, Waziri Mpango amesema kitendo hicho hakipaswi kuendelea kutokea, huku akiwapongeza wale waliohusika kwenye kufanikisha kukamatwa kwa madini hayo.

"Kwa niaba ya serikali napenda niwashukuru sana sana vyombo vyote ambavyo vimefichua uovu huu, ni unyama, mimi sina lugha nzuri ya kuwaambia mnataka niwaambie nini? ni unyama wa hali ya juu, ni ufisadi, hongereni sana kwa kutusaidia kufichua kujua tunaibiwa sana", alisema Waziri Mpango.

Waziri Mpango aliendelea kwa kuweka wazi jinsi hali ilivyokuwa wakati madini hayo yanakamatwa uwanja wa ndege, huku akisema kwamba zilisalia dakika 5 tu, ili ndege yenye madini hayo iondoke nchini, na ndipo walipoyakamata.

Madini yaliyokamatwa uwanjani hapo ni aina ya Almasi yenye thamani ya dola za Marekani milioni 29.5 iliyotambulika baada ya serikali kufanya tathmini yake, wakati yalipokamatwa wahusika walisema yana thamani ya dola za Marekani milioni 14. 7.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top