0


Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania  Mobile Tz ametuletea zawadi nzuri watanzania wote wapenda Burudani.
Baada ya kutoa Kitasa kisha Washa Tv na kuonekana kutofanya vyema,safari hii hapa ameamua kuumiza kichwa zaidi na kujua kuwa mashabiki wake wanapenda kitu gani.
Akizungumzia wimbo wake mpya Mobile ameuambia mtandao wa Walter Habari kuwa wakati anaingiza mashairi akiwa studio alijua kabisa kile anachokiimba kitagusa hisia za watu wengi.
Alisema ni wimbo alioumuza Kichwa usiku na mchana kwamba aandike mashairi gani na yenye ujumbe wa aina gani huku akitafakari ni nani atakayemshgirikisha kwa kuwa nyimbo zake mbili zilizopita yaani Kitasa na Washa Tv hakumshirikisha yeyote.
Mkali huyo wa miondoko ya R&B  ndani ya wimbo mpya unaojulkana kwa jina Tell me yaani niambie amemshirikisha mkali wa michano ya Hip hop Racka Rymes lengo ni kuwaletea burudani na ladha tofauti mashabiuki wa muziki wake.
Awali allipanga kufanya na Drizzy lakini baadae akaona pia Racka naye anafaa kwenye wimbo huo japo anao mpango wa kufanya kazi nyingine na Drizzy.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top