Baraza
la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), limelaani shambulizi la hivi
karibuni lililotekelezwa na watu wasiojulikana dhidi ya Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Mbunge
huyo aliyejeruhiwa Septemba 7 kwa kupigwa risasi tano mjini Dodoma,
hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan, jijini
Nairobi nchini Kenya.
Baraza pia limeungana na Watanzania kulaani kwa nguvu zote matendo yote ya vurugu, mauaji na uvunjifu wa amani nchini.
Tamko
la baraza hilo lililosainiwa na Makamu wa Rais wa TEC, Askofu Beatus
Kinyaiya limetolewa baada ya kikao cha kawaida cha baraza kilichofanyika
kwa siku mbili Septemba 9 na 10 jijini Dar es Salaam.
“Katika
Taifa letu sasa tunashuhudia matendo ya mauaji ya watu wasio na hatia
kama ilivyokuwa kule Mkuranga, Rufiji na Kibiti, utekwaji wa watu na
kuteswa, utekaji wa watoto, ulipuaji wa ofisi za watu na hivi karibuni
shambulio la mbunge Lissu,” limesema baraza katika tamko hilo.
Imeelezwa
vurugu na mashambulizi ya aina yoyote ile yanalifedhehesha Taifa kwa
kuwa matendo hayo ni dhambi, uhalifu na si utamaduni wa Mtanzania, hivyo
vyombo vinavyohusika havina budi kuyakomesha mara moja.
Post a Comment
karibu kwa maoni