Jeshi la polisi mkoa wa Manyara kwa kujali na kutambua umuhimu wa Michezo katika jamii wamekuletea Michuano ya soka itakayozikutanisha timu zisizopungua ishirini ndani ya mkoa.
Ligi itafunguliwa rasmi September 16 2017 ambapo inatarajiwa kuwa na mechi mbili kila siku katika vituo viwili,cha Magugu na Babati mjini uwanja wa Kwaraa.
Michuano hii ilikuwa ianze agosti 5 mwaka huu lakini zikatokea dosari hapo kati kati na kulazimika kusogezwa mbele.
Taarifa za uhakika ilizozipata JOHNWALTER HABARI ni kwamba michuano hiyo itaanza siku ya jumamosi na kufunguliwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Francis Masawe.
Uslama Cup kw mwaka huu imebeba Ujumbe mkubwa kwa jamii Katika kutii sheria bila shuruti,kupinga ujangili,kupinga mimba mashuleni, pamoja kutunza mazingira na misitu kwa lengo la kuifanya jamii iwe na uelewa wa mambo hayo muhimu.
Usalama cup 2017 imeandaliwa na kuratibiwa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali Maendeleo Mkoa wa Manyara.
Wadau hao ni:
EXPORT TRADE
CHEM CHEM
COMPANY
TANZANIA
POSTAL BANK TAWI LA BABATI
BAJWA
COMPANY
DODOMA
TRNPOT
POLE POLE
BUS SERVICE
FIRST AND
LAST BAR
MAFUNGU
AGROVET
CRDB BANK TAWI LA BABATI MJINI
MANUU
COMPANY
LALAA GALAPO
MAMA ANGO.
MATOKEO YOTE
LIVE ON WALTER HABARI,ARUSHA 24 NEWS NA JOHNWALTER BLOG
KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU NAMBA 0657932500
Post a Comment
karibu kwa maoni