Jumla ya watahiniwa 29,221 wakiwemo wavulana 13,461
na wasichana 15,760 wanatarajiwa kufanya
mitihani ya kumaliza elimu ya msingi katika Mkoa wa Manyara.
Afisa Elimu Taaluma Mkoa Lago Sillo, alisema kuwa watahiniwa hao wanatoka katika Wilaya za Kiteto,Simanjiro,
Hanang’, Mbulu na Babati na kwamba idadi
hiyo inahusisha watahiniwa wenye mahitaji maalum ya uoni hafifu, viziwi na
wasioona.
Alieleza kuwa
idadi ya watahiniwa kwa mwaka huu imeongezeka kwa watahiniwa 2982 ikilinganishwa na mwaka
jana ambapo watahiniwa walikuwa 26,239 wavulana wakiwa 11,737 na wasichana
14,502.
Akizungumzia kuhusu maandalizi ya mitihani hiyo
inayofanyika leo Sillo alibainisha kuwa
maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni ufanyaji wa mitihani ambapo aliwataka wasimamizi wa mitihani
kutenda haki kwa kufuata kanuni na taratibu za usimamizi wa mitihani.
Alifafanua kuwa wanafunzi wanafunzi 8,471 wakiwemo wavulana 5,357 na
wasichana 3,114 sawa na asilimia 22.4
wameshindwa kufanya mitihani kutokana na
mdondoko wa elimu.
“Mdondoko huo wa wanafunzi umesababishwa na utoro, kuhama hama kwa jamii
ya kifugaji hasa katika Wilaya ya Kiteto ambapo kumekuwa na asilimia 40 ya
utoro” alisema Sillo.
Alisema suala la mdondoko wa elimu
katika jamii ya kifugaji ni la mtambuka kwa kuwa jamii hizo hazitaki
watoto wao wasome na badala yake wachunge mifugo pamoja na matatizo ya
kifamilia.
Alifafanua kuwa wanafunzi walioanza darasa la
kwanza na wanaotarajiwa kuhitimu katika Wilaya ya Simanjiro ni wanafunzi 3,598
, Mbulu mji 2,952,Mbulu vijijini 3.919, hanang’6,281,Babati Mji 2,179 na Babati
Vijijini 6,946
Post a Comment
karibu kwa maoni