0


Image result for mkurugenzi wa babati MALINGA 
Ili kufikia adhima ya Serikali ya kutoa Elimu Bora,Wananchia wametakiwa kuendelea kuchangia miundo mbinu ya Elimua kwa hali na Mali katika maeneo yao, ili kupunguza upungufu wa Madarasa pamoja na Vifaa vya Elimu.
Hayo  yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Iddi Malinga wakati alipotembelea Ujenzi wa Madarasa 4, Offisi 2, Choo cha Matundu 12, katika shule Mpya ya Sekondari  Matufa .
Aidha Mkurugenzi  huyo amewaahidi Wananchi kuwa atatoa  Bati za kuezekea Jengo hilo, kwani lengo la Serikali  nikuwawezesha Wananchi na kuwaunga mkono katika Miradi mbalimbali ya maendeleo.
Sambamba na hilo Mkurugenzi huyo ametembelea ujenzi wa Bweni la Kidato cha tano  na Madarasa  2,pamoja na ukarabati wa madarasa 3, katika Shule ya Sekondari ya Mbugwe iliyopo Kata ya Mwada na kutoa wito kwa Viongozi kusimamia ujenzi huo kikamilifu.
Hata hivyo Serikali inaendelea kukabiliana na changamoto katika secta ya Elimu kwa kuwashirikisha Wazazi na Wananchi kuchangia kwa hali na mali Miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top