Wahamiaji waliorudishwa Libya kutoka
Nigeria watakwambia wamesikia visa vya kutisha vinavyowakumba safarini
wanapoelekea barani Ulaya kama vile utumwa nchini Libya, kuzama kwenye
bahari ya Mediterranean kabla hata kuihama nchi yao kujitafutia maisha
bora. Lakini hata habari hizo haziwezi kuwazuia wahamiaji waliojitolea.
Wahamiaji wengi hudhani hao hawatakumbana na bahati hiyo mbaya, amesema Josiah Emerole, kiongozi wa mawasiliano katika shirika la kupambana na ufasirishaji wa binadamu kinyume cha sheria nchini Nigeria.
Tabia hizo zimeanza kudhihirika enzi za mfumo wa Mila na tamaduni nchini Nigeria.
Kabla Ukristo na Uislamu kuwa Imani kuu nchini humo, raia wa Nigeria kama waafrika wengi waliamini kuwa kuna nguvu za giza ambazo zinaweza kudhibiti bahati ya mtu maishani.
Maelfu ya wahamiaji huvuka kuelekea Ulaya kila mwaka na hutuma fedha kwa familia zao kwa matumizi ya ujenzi nyumba na karo kwa ndugu zao kuendeleza masomo yao.
Post a Comment
karibu kwa maoni