0
Yanga itakuwa ugenini wikiendi hii kucheza dhidi ya Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom ndani ya Dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.
Licha ya kuwa ugenini, Yanga watamkosa kocha wao mkuu, George Lwandamina kutikana na kuwa na matatizo binafsi ya kufiwa na mwanaye.
Lakini huku nyuma, kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa amefafanua kuwa ili kupata matokeo mazuri katika mchezo huo watatumia mbinu ambazo wamachiwa na Lwandamina.
Yanga wakipata ushindi katika mchezo huo watatengeneza mazingira mazuri ya kuwa kuendelea kubaki katika mbio za ubingwa kwa kuwa wana tofauti ndogo kati yao na Simba ambao ndiyo wapo kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Nsajigwa ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania amesema kuwa wao wamekiandaa kikosi hicho kuhakikisha kinafanya vizuri katika mchezo huo na kuvunja mwiko wa kutoshinda mbele ya wapinzani wao hao katika msimu uliopita.
Msimu uliopita Mbao FC iliifunga Yanga mara mbili, kwanza ni katika Kombe la FA na katika Ligi Kuu ya Vodacom michezo yote ikiwa imechezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top