Rais wa Marekani Donald Trump
amemjibu Jay-Z baada ya mwanamuziki huyo wa muziki wa Rap kumuita "mdudu
hatari'' na kumkaripia kwa namna anavyowachukulia watu weusi.
Katika ujumbe kwenye Twitter Bw
Trump alisema kuwa "kiwango cha Wamarekani wasio na ajira kimeripotiwa
kuwa cha chini kabisa kuwahi kurekodiwa!" kwa sababu ya sera zake.
WaMarekani wenye asili ya Afrika
wasio na ajira ni asilimia 6.8%, kiwango ambacho ni cha chini kuwahi zaidi
kurekodiwa.
Lakini wakosoaji wanasema kuwa
kiwango cha ukuaji wa uchumi kilianza kuimarika wakati wa rais Obama na kwamba
ukosefu wa ajira miongoni mwa watu weusi umesalia kuwa wa kiwango cha juu
miongoni mwao kuliko miongoni mwa wazungu.
Alipokuwa katika kipindi cha
televisheni ya CNN cha Van Jones Show, Jay-Z alisema kuwa kuangazia viwango vya
ukosefu wa ajira ni " kukosa ufahamu wa mambo".
"Sio suala la ukosefu wa pesa
pekee lenye umuhimu … pesa hazileti furaha... hazileti. Hii ni kushindwa
kuelewa ukweli. Uwachukulie watu kama binadamu ...hilo ndio suala kuu la
muhimu."
Aidha amesema kuwa kuchaguliwa kwa
Bw Trump kulitokana na kushindwa kutatuliwa kikamilifu kwa masuala kadhaa.
"Umepuliza manukato katika debe
la taka," alisema. "Unapofanya hivyo ni kwamba unawafanya wadudu
hatari kufika. Unapopuliza kitu basi unasababisha kuzaliwa kwa wadudu hatari
kwa sababu haungazii tatizo halisi."
"Hauchukui taka nje, unaendelea
kupuliza dawa juu yake ili kulifanya debe la taka kukubalika. Vitu hivyo vinapokuwa,
huwa unabuni mdudu hatari . Na kwa sasa mdudu hatari tuliyr naye ni Donald
Trump, mdudu hatari."
Jay-Z alimuunga mkono Barack Obama
wakati wa uongozi wake, na alimsifia Bi Hillary Clinton katika uchaguzi wa
mwaka 2016 ambapo Bwana Trump alishinda
Pia aliulizwa kuhusu madai ya rais
Trump kuyataja mataifa ya Afrika kuwa "machafu" au mataifa ya
"mabwege"
Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa
vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile
Botswana na Ghana.
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa
@realDonaldTrump
Bw Trump amekanusha kwamba alitumia
neno hilo kuyaelezea mataifa ya Afrika.
Hata hivyo alikiri kwamba alitumia
maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa
anazungumzia wahamiaji wanaoingia Marekani.
"Inasikitisha na
inaumiza," alisema Jay-Z. "Kila mtu anahisi hasira. Baada ya hasira,
inasikitisha sana kwa sababu ni kama ana dharau kwa watu wote ."
Rais Trump amekanusha madai yote
kwamba ya ubaguzi dhidi yake.
Alisema kuwa lugha aliyoitumia
ilikuwa ni ya ''ukali '' lakini anakana kutumia neno linaloripotiwa.
Post a Comment
karibu kwa maoni