
Mwenyekiti
wa Bodi ya Parole Tanzania, Augustino Mrema amelitaka Jeshi la Polisi
na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kumchukulia hatua aliyezusha
taarifa za kifo chake Januari 9 mwaka huu.
Mrema
ambaye ni Mwenyekiti wa TLP Taifa ameyasema hayo mapema leo alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari nje ya Kituo cha Polisi jijini Dar es
Salaam alipokwenda kuripoti tukio hilo.
Amesema,
aliyezusha taarifa hiyo alifahamu kwamba Lowassa amekwenda Ikulu
kuonana na Rais Dkt Magufuli, hivyo akazusha uongo ili watu wasiwe
makini kuhusu kilichojadiliwa Ikulu.
Mrema
amesema wapinzani wa Rais ndio walizusha taarifa hizo za uongo na kuzua
taharuki kwa sababu yeye ni mtu maarufu na wanajua kwamba kwa kufanya
hivyo wangesababisha watu kutofautilia kilichozungumza Ikulu.
Baada
ya kusema hayo, Mrema ameweka wazi kwamba anataka kulipwa fidia ya TZS
20 bilioni kutokana na kuzushiwa kifo na kwamba fedha hiyo haitapungua
hata shilingi mia.
Post a Comment
karibu kwa maoni