0
Mshambuliaji wa Azam FC Mbaraka Yusuph amekaribia kurejea kwenye kikosi baada ya kupona majeraha yake na kuanza programu ya mazoezi mepesi peke yake.
Hayo yamebainishwa leo na Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Abdulkarim Amin wakati akiongelea safari ya Azam FC kuelekea mikoa ya Ruvuma na Mbeya kwaajili ya mechi mbili za ligi kuu.
''Benchi lote la ufundi likiwa na watu 10 limeondoka leo alfajiri na kikosi cha wachezaji 25 isipokuwa Mbaraka Yusuph ambaye alikuwa majeruhi lakini amerudi kutoka Afrika Kusini na anaendelea na mazoezi binafsi kabla ya kuungana na timu'', amesema Abdulkarim.
Aidha Abdulkarim ameongeza kuwa nyota wengine waliokuwa majeruhi Shabaan Idd Chilunda na Joseph Kimwaga tayari wamepona na wamesafiri na kikosi tayari kwa kucheza.
Azam FC ikiwa Ruvuma itacheza na Majimaji FC kwenye mchezo wa raundi ya 13 alhamisi hii kisha itaelekea Jijini Mbeya kucheza na Mbeya City kwenye mchezo wa raundi ya 14 ligi kuu soka Tanzania.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top